Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Nurudini Bilal , amesema Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imetenga shilingi bilioni 2.1 kwa ajili ya maswala ya mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi wilayani Ilala.
Meya Nurudini Bilal , amesema hayo Dar es Salaam katika mafunzo ya siku mbili ya Mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yameandaliwa na Taasisi ya C 40 ya Uingereza na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambayo imeshirukisha Halmashauri za mkoa Dar es Salaam.
“Halmashauri yetu ya jiji la Dar es Salaam katika bajeti yake imetenga shilingi bilioni 2.1 na shilingi bilioni 6.7 tumetenga kwa ajiii ya kukusanya taka ndani ya jiji letu sababu takataka sio chanzo cha mapato katika jiji letu “alisema Meya Nurudini
Meya amesema hivi karibuni alikuwa Afrika Kusini katika mafunzo kujifunza maswala mbalimbali ambapo amesema katika uongozi wake anapenda kuwa na jiji safi anatamani kuwa na jiji safi na salama .
Aidha amesema mafunzo hayo yanaenda kuwajengea uwezo katika kufanya vizuri kwenye mabadiliko ya tabia ya nchi.
Meya amesema mpango waliozindua leo wa Kitabu cha taka na kitabu cha Nishati katika mabadiliko ya tabia ya nchi katika uongozi wake wa miaka mitano utaenda pia kutoa ajira ya fursa kwa vijana 300 Halmashauri ya jiji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya, amesema Halmashauri hiyo ni siku muhimu na Wataalam wake wa Mazingira yanayotunzwa yawe endelevu sambamba na viumbe hai.
Mkurugenzi Elihuruma Maberya ,amesema Ilala wanazalisha takataka tani zaidi 4600 na zinazosafirishwa 2600 alipongeza mpango huu wa mabadiliko ya tabia ya nchi takataka iwe sehemu ya ajira.
Amesema takataka ni bidhaa uzalisha hewa ya kabon mpango huu unakwenda kuibadili Halmashauri ya jiji hilo kwenda kuwa safi na kuvutia.





