Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Serengeti
MKUU wa Wilaya ya Serengeti Kemlembe Ruota amesema kuwa wanasubiri taarifa kamili kutoka timu ya uchunguzi ya mgogoro wa ardhi uliopo kwa takribani miaka 17 kati wananchi wa Kata ya Kisaka na Jeshi la Wananchi JWTZ kikosi cha Makoko FARU JK 27.
Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya hiyo ya Serengeti imekuja baada ya baadhi ya Diwani ya Kata ya Kisaka kumuomba Mh Rais Dkt Samia Suluh Hassan kuingilia kati mgogoro na kuwarudishia eneo lao ambalo linasemekana Jeshi hilo limetwaa bila ya kuwashirikisha wanakijiji wa vijiji ivyo 5.
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo amesema timu iliyoundwa itakuja na jibu kamili kwani hata wao wanashindwa kuingilia kutokana na Jeshi na Wananchi wanaoishi hapo wote ni Serikali.
“Kwa sasa tuache timu iliyoundwa ifanye kazi yake na baada ya kumaliza itatupa jibu kamili kuwa nani ni mmiliki wa eneo hilo na ukubwa gani kati ya Jeshi la Wananchi au wanakijiji wa vijiji ivyo 5 ambavyo vinadai kuwa Jeshi hilo limetwaa eneo hilo”amesema Mkuu wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya hiyo, alisema kuwa mchakato mzima unaonyesha kuwa Jeshi wanamiliki ardhi hiyo huku baadhi ya wanakijiji wa Nyiboko wakisema kuwa waliwakaribisha Jeshi hilo kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kijeshi mnamo mwaka 2008.
Kwa upande wake ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Ayoub Makuruma amewataka Wananchi wa Kata ya Kisaka kuwa watulivu kwa kipindi hiki huku timu ya wataalamu ikiwa inafanya kazi na kuchunguza juu ya makubaliano ya awali yaliyoingiwa kati ya Kijiji cha Nyiboko na Jeshi la Wananchi JWTZ.
Katika makubaliano ya awali unaonyesha kuwa Jeshi la Wananchi (JWTZ) yameonyesha kuwa waliingia makubaliano kati Jeshi la Wananchi na viongozi wa Kijiji cha Nyiboko walikubaliana ila kinacholalamikiwa kuna baadhi ya maeneo hayakuwa katika makubaliano hayo ndio yamegeuka kuwa changamoto na kuleta mgogoro huo wa ardhi kwa mda mrefu.
“Timu zinafanya kazi tuache zifanye kazi Ili baada ya apo tutakuwa na pakusemea baadae tutajua ukweli”amesema Makuruma.
Kupata majibu yaliyojitosheleza kutoka kwa timu ambazo zinaendelea kufanya kazi na kuwa Serikali ni Moja kati ya Wananchi na Jeshi basi Kijiji cha Nyiboko waliotoa eneo kwa ajili ya Jeshi la Wananchi JWTZ kufanya mazoezi kwa mujibu wa wakazi wa Kijiji hicho.

“Hatuwezi kuwa na majibu ya mojakwa moja kuwa eneo hilo ni la Wananchi au Jeshi la Wananchi bali niwasihi wakazi wa Kata ya Kisaka kuwa watulivu huku tukisubiri majibu kutoka kwa timu iliyoundwa”.amesema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Serengeti.
Pia, Mwenyekiti huyo amesema kuwa atuwezi sema kuwa viongozi waliopita wa kijiji cha Nyiboko kuwa walikuwa na makosa au Halmashauri kwa kuwa muhtasari wa vikao wa kugawa eneo hilo upo.
Ameongezea kuwa, kinachoendelea sasa ni kutambua kiasi gani cha ardhi walichopewa na kipo kwenye vikao vya Kijiji na kwa uelewa wangu Kijiji kutoa ekari 40 nj sehemu ndogo kwa JWTZ labda iwe kwa ujenzi wa Nyumba za kuishi na sio sehemu ya kufanyia mazoezi ya kijeshi.
Ekari 40 ni ndogo sana kwa kuweka kambi kwa Jeshi kwani mara nyingi kambi hizo zinakuwepo na sehemu ya kulengea shabaha na kupiga mizinga.
Naye , Mwenyekiti wa Kijiji cha Marembota William Sibaire akiongelea mgogoro huo alisema kuwa mnamo mwaka 2008 Jeshi la Wananchi (JWTZ) liliingia katika eneo la kata ya Kisaka kufanya mazoezi ya kijeshi ndipo baadhi maafisa wa( JWTZ )wakaanza kusema kuwa wamependezewa na sehemu hiyo na watakuwa wanarudi mara kwa mara kufanya mazoezi ya kijeshi .
Pia, Mwenyekiti akaeleza kuwa kuingia kidogo kidogo kwa kufanya mazoezi ya kijeshi ya kupiga mizinga na kulenga shabaha na wanakijiji walikuwa wanapewa huduma za kijamii za kupima afya bure na kurahisisha kazi ya kikosi hicho kutwaa eneo hilo .
Hata hivyo baada ya kuliona eneo hilo linafaa ndipo waliwaambia baadhi ya wanakiji wa kata ya Kisaka kuwa watakuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi na kuwahadaha watawajengea hospital.
Baada ya Jeshi kulichukia eneo hilo la vijiji ivyo kumekuwa na madhara na athari za mabomu,risasi na mizinga inavyoungurishwa wakati wa mazoezi na kusababisha baadhi ya wazee kupata mshtuko wa ugonjwa wa moyo , wengine kujawa na hofu , wazazi mimba kuharibika na baadhi ya wanyama kufa wakiwa malishoni.
Mwanzo Jeshi la Wananchi (JWTZ) lilipewa ekari 40 za kufanyia mazoezi huko Nyiboka na waliokuwa viongozi wa kwa wakati huo Marwa Nkombi kutoka Nyiboka, Diwani aliyepita Elisha Makaiga na Daudi Marimbeta wa nyiboko ndio waliotoa eneo hilo kwa Jeshi la Wananchi JWTZ kwa kisingizio kuwa eneo hilo limekithiri kwa wizi.
Na kusisitiza kuwa bado wanalihitaji eneo hilo kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo na uwepo wa kambi ya Makoko ni shida iliyopo kwa mda mrefu.
“Wamezuia wanakijiji kulisha mifugo yao wala kupita eneo hilo na ndio njia kuu au Barbara ya kupita kwenda wilayani na kwenda kata nyingine za karibu pia ikafikia baadhi ya wananchi kupigwa kwa mara kwa mara ” amesema Sibaire.
Na katika eneo, lililobaki limepitiwa na Mto mara na mara mvua zinaponyesha husababisha mafururiko kutoka kwenye mto huo kutokana na mvua zinazonyesha kutoka maeneo ya Mkoa wa Arusha na nchi jirani ya Kenya kutokana na bonde la mto mara kupakana na Mto huo.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kijiji kwa Nyiboko Masugo Maro , amesema kuwa kijiji hicho ndicho kimeathirika mno kutokana kuwepo kwa kambi ya Makoko kutokana na baadhi ya viongozi wa kambi mwaka Jana kuja na kuweka alama za utambuzi wa ardhi (B.con) kwenye maeneo ya watu bila ya kuwashirikisha wanakijiji na kuwapa wakati mgumu viongozi kujibu maswali ya Wananchi juu ya zoezi hilo.
Pia, matumizi ya silaha kubwa wakati wa mazoezi na kuharibu nyumba za makazi ya wanakijiji na wakati mwanzoni wanakuja tuliwapa kwa nia njema ya kufanya mazoezi na mbaya zaidi sasa wamewazuia wanakijiji kufanya shughuli zao kwenye maeneo yao.
“Mwanzoni wanakijiji waliokuwa wanaokaa kwenye eneo hilo walikuwa wanafanya shughuli zao na sasa wamewazuia kufanya ivyo “amesema Mwenyekiti Maro.
Kuna wakati mkuu wa Mkoa wa Mara akiwa Adam Malima alikuwa anafunga mafunzo ya kijeshi baadhi ya wanakijiji walikuwa wanalalamika kutolewa kwenye maeneo yao ndipo mkuu wa Mkoa akataka maelezo ya jinsi Jeshi hilo wamepatake sehemu hiyo kubwa katika vijiji ivyo na aliomba muhtasari wa ukubwa wa eneo na mipaka yake ikoje lakini hakuwai pelekewa ripoti hiyo.
Kuna taarifa kuwa baadhi ya viongozi kwenye eneo hilo wamegawana na kuweka mifugo bila ya kufuata taratibu karibu na kambi na baadhi ya wananchi wamefatilia kuanzia viongozi wa vijiji ,kata wilaya mpaka Mkoa bila ya kupata majibu” amesema Maro.
Wenyeji na wadau wote wa Kata ya Kisaka walio ndani ya nchi na nje ya nchi washirikishwe katika mchakato mzima wa utowaji wa eneo na maamuzi yao yaeshimiwe.
Pia, wananchi na viongozi wao wameomba kuaniasha tathmini na athari za sehemu hiyo ya utoaji wa eneo hilo kwa Jeshi la Wananchi (JWTZ )sababu hata viongozi wa juu wa kambi hiyo waliopita walishawai kusema kuwa sehemu hiyo sio rafiki tena kutokana na kuwepo kwa makazi ya Wananchi.