Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Sumbawanga Mjini Frank J. Maten, amekabidhi fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa Edwin Matondwa Kachoma mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo.
Kachoma amesema kuwa anaimani atapata nafasi ya ubunge katika Jimbo hilo huku akiwataka wananchi kutimiza haki yao ya msingi.
