Mgombea Uwakilishi Jimbo la Makunduchi, Haroun Ali Suleiman amesema mgombea urais wa Chama Chama Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan na mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi wamefanya kazi kubwa ya maendeleo.
Suleiman amesema hayo leo Septemba 17 katika mkutano mkubwa wa kampeni za urais katika viwanja vya Kajengwa Makundunchi mkoa wa Kusini Unguja.
“Mmefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo, tumeshuhudia ujenzi wa shule za ghorafa, barabara na maji kila eneo.
“Mmetuliza nchi pande zote mbili zimekuwa na amani na utulivu mkubwa, ndiyo maana tunashuhudia maendeleo hayao,”amesema.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya kazi kubwa, ikiwamo ujenzi wa barabara kutoka kisiwa cha Uzi kwa kiwango cha lami kwa mara ya kwanza katika hiyo ya Zanzibar.



