Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi (kulia) amemkabidhi fomu ya uteuzi mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman leo Agosti 31, 2025.
Othman anayegombea kupitia Chama cha Act-Wazalendo, amekabidhiwa fomu katika Ofisi Kuu ya ZEC iliyopo mtaa wa Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.
