Wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Manzese Bakresa, kushuhudia uzinduzi wa kampeni za ubunge wa mgombea wa Jimbo la Ubungo, Queen Julieth Lugembe.

Katika uzinduzi huo mgombea Queen Julieth alizungumza na wananchi wa jimbo hilo, akieleza ahadi zake na mipango yake ya maendeleo endapo atapata nafasi ya kuliongoza Jimbo la Ubungo .