Mgombea wa nafasi ya Rais na Mwenyekiti CCM Taifa Dk Samia awasili Iringa
JamhuriComments Off on Mgombea wa nafasi ya Rais na Mwenyekiti CCM Taifa Dk Samia awasili Iringa
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa Septemba 07, 2025 kuzungumza na wananchi ili kuwaelezea sera za chama chake na. kuwaomba kura za ndiyo kuelekea uchaguzi mkuu, utakaofanyika Oktoba 29, 2025 mwaka huu.Chifu wa Kabila Wahehe Adam Abdul Adam Sapi Mkwawa wa pili akimkaribisha Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Kalenga mkoani Iringa katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani humo tarehe 06 Septemba, 2025. Chifu huyo wa Kabila la Wahehe alisimama katika eneo la Kichuguu cha Kidundaa ambalo Chifu wa Kabila hilo Mtwa Mkwawa alikuwa akilitumia wakati akizungumza na watu wake wa Kalenga.