Na Mwandishi Wetu,Jamhuri Media-Songea

Waziri wa Afya na mgombea ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama amesema mgombea Rais Samia Suluhu Hassan ameandika historia ambayo haitafutika kizazi na kizazi kwa kumteua Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza.

Amesema uteuzi huo ni heshima kubwa kwa wananchi kwenye wa Mkoa wa Ruvuma na Watanzania kwa ujumla.

Amesema Rais Samia alipoingia madarakani mwaka 2021, nyuso za wana Peramiho zilikuwa na masikitiko makubwa ya bei ya mbolea kuwa juu.

Amesema wakati huo mfuko mmoja wa mbolea ulikuwa unauzwa Sh150,000, lakini kazi nzuri iliyofanywa na Rais Samia bei imeshuka hadi Sh 70,000.

“Wananchi walikuwa na masikitiko makubwa mno, umefanya kazi nzuri, sasa mfuko unanunuliwa shilingi 70,000, huu ni ukombozi kwetu wana Songea,”amesema.

Amesema uzalishaji wa chakula katika mkoa huo ni ajenda ya uchumi ambayo mpaka sasa imeongeza uzalishaji kutoka tani milioni 1.3. mpaka milioni 1.7.

“Haya ni mapinduzi makubwa mno mheshimiwa mgombea, hali imesaidia wakulima wetu na Taifa zima,”amesema.

Sehemu ya umati wa wananchi wa Songea waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma tarehe 22 Septemba, 2025, Mkutano uliohudhuriwa kwa pamoja na Mgombea Mwenza Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi pamoja na Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Amesema pamoja na yote hayo,ruzuku ya mbolea imefanya vijana wengi kununua pikipiki maarufu bodaboda na kuwapa ajira.
“Tuko na wewe mpaka kieleweke, Oktoba 29 tunatiki, tunatiki,tunatiki,”amesema.
Kuhusu miundombinu, Mhagama amesema serikali imefanya maboresho makubwa hasa sekta za miundombinu.

Amesema wamejengewa hospitali za wilaya, zahanati na vituo vya afya ambazo zimejengwa vyumba maalumu kwa ajili ya kina mama.

wejengwe hospitali kwenye wilaya.

Amesema huduma za afya zimepunguza vifo vya kina mama kutoka 556 hadi 114 kwa Jimbo la Perahimo.


‘Hakuna jambo linalotugusa bila kujali itikadi za vyama siasa, Oktoba tunatiki.

Amesema miundombinu imeimarishwa kwa kujenga maghala 11.