Tanzania tunapoadhimisha leo miaka 26 bila ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Amani na umoja ndizo tunu muhimu alizotuachia na zikisimamiwa kikamilifu na kwa nguvu kubwa na Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiamini kwamba umoja ndiyo nguvu ya mnyonge na amani ndilo chimbuko la maendeleo na ustawi wa Mtanzania na Taifa kwa ujumla.
Wakati chimbuko hilo la maendeleo ikitikiswa na watu wenye mtazamo tofauti kuhusu uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia, mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania mara zote tumemsikia akizungumza, kutoa miito ya ulinzi na kukumbusha kuhusu wajibu wa kila mmoja katika kulinda amani ya Tanzania, akisema siasa na uchaguzi havipaswi kuwa silaha ya kuangamiza amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.
Kama ambavyo anasisitiza na kueleza dhamira yake ya kulinda tunu za Taifa na kutunza mema tuliyoachiwa na Baba wa Taifa.
