Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Moshi
Mgombea ubunge Jimbo la Rombo, Profesa Adorf Mkenda amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Sh bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Chala.
Ametoa kauli hiyo alipopewa nafasi ya kusalimia maelfu ya wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwaani kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro leo Oktoba,2025.
Amesema mradi huo utasaidia kumaliza tatizo la maji ambalo lilikuwa linawasibu wananchi wa wilaya hiyo.

Pia amesema kujengwa kituo cha forodha katika mpaka wa Horiri na Tarakea kumesaidia wafanyabiashara kufanya kazi saa 24.
“Sasa hivi ni burudani tosha mheshimiwa, wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa saa 24, hii inasaidia kuongeza pato la Taifa,”amesema.
Pia amesema ujenzi wa barabara na soko kubwa vitasaidia kuondoa changamoto zilizokuwapo.
kuhusu amesema wanataka wawe na kilimo cha kimataifa cha ndizi kutokana na wilaya hiyo kuwa kinara wa uzalishaji ndizi.
‘Tunataka kilimo cha ndizi kiwe cha kimataifa, tunaomba tuwe na kilimo cha umwagiliaji wa matone,”amesema.
Kuhusu hospitali ya wilaya amesema tayari na imeanza kutoa huduma.
