Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Uvinza

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, John Mongela, amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea mgombea urais wa chama hicho, Samia Suluhu Hassan ili awe na afya njema.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma Leo Septemba 13, Mongela amesema kazi kubwa ya maendeleo yanayoonekana sasa ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia.

Amesema amejitahidi kupambana na umasikini na kuinua hali ya maisha ya Watanzania.

“Nawaomba kila mmoja wenu amuombee Rais wetu awe na afya njema, amefanya kazi ya kuleta maendeleo ndani ya miaka minne hii,”amesema.