





engo la gorofa tisa linalomilikiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF), lililopo eneo la Posta jijini Dar es Salaam, limenusurika kuungua baada ya moto kuibuka na kusababisha hataruki kubwa.
Taharuki hiyo imetokea leo Januari 16, 2026 majira ya saa sita na kusababisha vurugu kutokana na watu kukimbia kwa nia ya kujiokoa ambapo chanzo chake bado hakijafahamika.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama, limefanya jitihada za kuzima moto huo pamoja na kuwaokoa watu waliokuwepo ndani ya jengo hilo.

