Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Buhigwe
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema ameitendea haki Ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo Septemba 13 wilayani Buhigwe alipopewa nafasi ya kusalimia mamia ya wananchi na kumnadi mgombea wa chama chake.
“Mgombea wetu ameitendea haki Ilani ya CCM ya mwaka 2000/25, amefanya makubw sana, kila mmoja wetu anajionea kwa macho yake ndani ya Wilaya yetu, ombi langu kwenu wote tuliojiandikisha twendeni kwenye kituo cha kupiga kura tumpigie Rais Samia ili apate nafasi ya kuendelea kuijenga nchi yetu.
“Naungana na wana Kigoma kukuombea maisha mema na maisha marefu ili Buhingwe iendelee kung’aa najua mambo mengine yapo katika ilani utaendelea kuyafanyia kazi kama kawaida yako,”amesema.
Amemshukuru Rais Samia kwa kumteua kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kipindi chote alichofanya naye kazi.
