Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. ๐ฆ๐ฎ๐บ๐ถ๐ฎ ๐ฆ๐๐น๐๐ต๐ ๐๐ฎ๐๐๐ฎ๐ป iwapo atapewa kura za kutosha na kupata ridhaa ya kuongoza tena kwa miaka mitano ijayo atadumisha na kuongeza juhudi za kuimarisha huduma za afya mkoani Kilimanjaro na nchi nzima kwa ujumla.
Dkt. Samia amesema dhamira yake ni kuhakikisha kuna utoshelevu wa dawa muhimu katika vituo vya afya, kuongeza watumishi wa afya na vifaa tiba katika hospitali na vituo vyote nchini.

Akihutubia maelfu ya wanachi wa Moshi katika viwanja vya mashujaa, Ameyasema haya;
โKatika kipindi changu cha kwanza cha uongozi, tumefanikisha kuongeza upatikanaji wa dawa nchini kufikia asilimia 86.”
“Kazi hii itaendelea zaidi ikiwa nitapewa ridhaa ya kuongoza serikali kupitia uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025”
Pia, Dkt. Samia ameeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa miaka 5 iliyopita ambapo amegusia maboresho makubwa yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro, ikiwemo huduma za wagonjwa mahututi, usafishaji wa figo, huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda pamoja na vipimo vya kisasa.

Aidha, amekumbusha uzinduzi wa jengo la mama na mtoto aliloufanya katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu ya sita.
Dkt. Samia ameweka wazi kuwa uwepo wa jengo hilo umewezesha ongezeko la idadi ya akinamama wanaojifungulia hospitalini katika mkoa wa Kilimanjaro kutoka 260,486 hadi 328,502, hatua ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya uzazi.
Huu ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Urais mkoani Kilimanjaro ambazo zilianzia jana wilayani Same na zinahitimishwa leo tarehe 1 Oktoba 2025 ambapo pia Dkt. Samia atawasili na kupokelewa mkoani Arusha.



