Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Greyson Msigwa, amewataka waandishi wazalishaji habari mtandaoni kutambua kuwa dunia ya vita yake haitumii silaha za kijeshi bali imehamia kwenye taarifa kupitia mitandao ili kujaribu taswira chanya kwa wananchi

Ameyasema hayo leo Desemba 18,2025 katika kikao kazi na wnahabari jijini Dar es Salaam amebainisha kuwa Tanzania kipindi kugumu Taifa kikichopitia ni sababu ya taarifa zilizokuwa zikienea kupitia mitandao ya kijamii hivyo licha ya zana iliyokuwa inayosemwa kuwa waandishi Watanzania ni wadhaifu lakini mlionyesha uzalendo wa utaifa wenu kwa kutotumia kalamu zenu vibaya kuwa miongoni mwa wachochezi.

“Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani inawapongeza sana mesisitiza kuwa waandishi wa habari wa mitandaoni kuwa ni sehemu muhimu ya ulinzi wa taifa katika dunia ya sasa, ambapo mapambano makubwa hayatumii tena silaha za kijeshi bali taarifa na mitazamo ya wananchi”amesema Msigwa.

‎Msigwa ameongeza kuwa katika mazingira ya sasa ya kimataifa, taarifa potofu, propaganda na matumizi mabaya ya mitandao vinaweza kudhoofisha taifa endapo havitadhibitiwa kwa weledi na uzalendo.

‎“Leo vita vimehama kutoka bunduki na hadi kwenye taarifa. Waandishi wa habari mnayo nafasi kubwa ya kuilinda nchi yetu kwa kalamu na majukwaa yenu,” amesisitiza Msigwa.



Aidha ‎ameeleza kuwa serikali imechagua mkakati wa kushirikiana na wadau wa habari, hususan waandishi wa mitandaoni, ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu wajibu wao wa kitaifa badala ya kutumia nguvu za kisheria pekee.

‎Katika hatua hiyo, ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuendelea kuchukua mwelekeo wa kuwajenga na kuwaongoza waandishi wa mitandaoni, akisema njia hiyo inaleta matokeo chanya kwa taifa.

‎Msigwa ameitaja Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jukwaa la Mitandao Tanzania (JUMIKITA) kuwa ni washirika wakuu wa serikali katika mapambano ya taarifa, akisisitiza kuwa mchango wao unaisaidia serikali kuwafikia wananchi na dunia kwa ujumla.

‎“Serikali imewaamini hivyo ni wajibu wenu sasa kuhakikisha majukwaa yenu hayatumiki kuichafua nchi, bali kuitangaza na kuilinda,” ameongeza.

‎Pia amekanusha hoja kuwa waandishi wa mitandaoni hawana uwezo au weledi, akisema wengi wao wameonyesha uzalendo mkubwa na taaluma ya hali ya juu katika kazi zao.



‎Kwa upande wa mazingira ya kazi, Msigwa amewahakikishia waandishi kuwa serikali iko tayari kurekebisha sheria, kanuni au sera zitakazobainika kukwamisha mchango wao katika maendeleo ya taifa.

‎Aidha, ametangaza kuwa serikali kwa kushirikiana na TCRA inaandaa mafunzo maalum ya uzalendo wa kidijitali na weledi wa habari, yatakayolenga kuwawezesha waandishi kukabiliana na changamoto za taarifa potofu na propaganda.

‎Kuhusu masuala ya kodi, Msigwa amesema serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutatua changamoto za kikodi, akitambua mchango wa waandishi wa mitandaoni katika kuitangaza Tanzania na kuvutia uwekezaji.

‎Awali, Mkurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Kuwe amesema wataendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa wazalishaji wa maudhui mtandaoni ili kuwawezesha vijana kujiajiri, kukuza uchumi wa kidijitali na kulitangaza Taifa kwa mlengo chanya.



‎Vile vile ameongeza Kwa kusema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa wazalishaji wa maudhui mtandaoni katika kusambaza taarifa, kuitangaza nchi na kufungua fursa za ajira kwa vijana, hivyo imeamua kuweka mifumo rafiki itakayowawezesha kuanza kazi bila vikwazo vikubwa vya kifedha.

‎Amebainisha kuwa hadi sasa TCRA imeweka utaratibu maalum unaomruhusu mwandishi mtayarishaji wa maudhui anayeanza kujitokeza kuomba kufanya shughuli zake kwa kipindi cha miezi mitatu bila kulipia ada yoyote, ili kumpa nafasi ya kujijenga na kuelewa taratibu za kazi.

‎“Lengo letu si kuwabana vijana, bali kuwawezesha. Tunataka waingie kwenye tasnia kwa utaratibu mzuri, wajenge uwezo wao na baadaye wachangie kikamilifu kwenye maendeleo ya Taifa,” amesema Kuwe

‎Kwa mujibu wa TCRA, maboresho hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kujenga uchumi wa kidijitali unaowapa vijana fursa za ajira na kukuza tasnia ya habari nchini.