Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia,Singida
Mbunge wa Jimbo la zamani la Singida Mashariki, Miraji Jumanne Mtaturu, leo ameweka wazi nia yake ya kuendelea kulitumikia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo Jipya la Ikungi Mashariki.
Hatua hiyo imekuja baada ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kutangaza rasmi mabadiliko ya majina ya baadhi ya majimbo ya uchaguzi, ambapo Jimbo la Singida Mashariki sasa limegawanywa na kuitwa Ikungi Mashariki, huku upande mwingine ukibeba jina la Ikungi Magharibi.
“Nimeitikia wito wa wananchi na wanachama waliotamani niendelee kusimama kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Ikungi Mashariki,hii ni safari ya kuendeleza kazi tuliyoianza kazi ya kuimarisha huduma za jamii, na kusimamia haki za wananchi bungeni,” amesema Mtaturu.

