Na Magrethy Katengu -JamhuriMedia,
Dar es Salaam

Katika kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislam 1447 Wananchi wameshauriwa kuhudhuria Viwanja vya Mnazi Mmoja kupata huduma katika Maonyesho Muharram Expo ikiwemo huduma za Afya bure,Elimu ya Kifedha,na kutoa
damu.

Akizungumza na waandishi wa habari ,Jijini Dar es Salaam Kiongozi Mwandamizi wa Taasisi za Kiislamu Tanzania, Mohamed Issa, amebainisha kuwa Mwaka Mpya wa Kiislam Muharram utaambatana na maonesho ambayo yatahudumia jamii kiafya ikiwa ni ishara ya kujali na upendo.

“Maonesho haya ambayo yameanza Jumanne wiki hii na yatahitimishwa baada ya siku saba tunawaalika wananchi wenye changamoto za kiafya wafike watahudumiwa ,elimu ya kisheria zitatolewa , kifedha na namna kutunza fedha ,” amesema.

Pia amesema wananchi watapewa elimu kuhusu huduma za masoko ya mitaji na dhamana na uwekezaji wa pamoja (Collective Investment Schemes) isiyo na riba kama vile mifuko ya Uwekezaji Halal au Halal Fund, hati fungani zisizo na riba inayofahamika kama Sukuk.

Naye Amiri wa Baraza Kuu la Kiislamu, Sheikh Mussa Kundecha, amebainisha kuwa maonesho hayo si kwa ajili ya waislamu pekee bali ni kwa Watanzania wote hayabagui kujali dini .

“Ndio maana tumeyaweka katika viwanja hivi vya Mnazi Mmoja eneo la wazi ili kila mwananchi afike kupata huduma hususani wafanyabiashara ambao watapata elimu sahihi kuhusu mikopo,” amesema.

Aidha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemani Jaffo, anatarajia kuwa mgeni rasmi kutembelea maonesho ya pili ya Huduma za Kifedha na Kijamii ‘Muharram Expo’ yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.