Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Kibaha
Aliyekuwa Mwekahazina wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Abubakar Alawi, leo Juni 30, 2025, amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Fomu hiyo imekabidhiwa kwake katika ofisi za CCM Kibaha Mjini na Kaimu Katibu wa chama hicho, Joel Kituu.
Hii ni mara ya pili kwa Mwalimu Alawi kuwania nafasi hiyo, baada ya kujaribu kwa mara ya kwanza mwaka 2020, ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 88, nyuma ya mshindi wa nafasi hiyo, Silvestry Koka.


