Maelfu ya wananchi wa Mwanza wamempokea Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, na kumpa salamu zao ya kwamba wamejipanga vema na wapo tayari kumpokea Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 08 Oktoba 2025.

Dkt. Samia atanadi Ilani ya CCM (2025/30) , Sera na Ahadi zake pamoja na kuomba kura katika kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29.