Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mwenge wa Uhuru wazindua miradi saba ya maendeleo Wilayani Ilala yenye thamani ya shilingi bilioni 44.1 na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Isimail Ally Ussi. 

Akizungumza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alitaja miradi hiyo kuweka jiwe la msingi la Nishati safi soko ls samaki Feri wilayani Ilala.

 

“Mwenge wa Uhuru leo umezindua miradi saba ya maendeleo Wilaya ya Ilala yenye thamani ya shilingi bilioni 44.1 na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Isimail Ally Ussi “alisema Mpogolo. 

Mpogolo alitaja miradi mingine kuwa ni kuweka jiwe la msingi barabara ya Tabata Magengeni kutembelea mradi wa kiwanda kidogo cha kutengeza samani unaotekelezwa na kikundi cha Vijana Ulipo Tupo Segerea. 

Aidha alitaja miradi mingine kuwa ni kutembelea na kuweka jiwe la msingi kiwanda cha usambazaji maji Pugu mwa Dar es Salaam eneo la Pugu Stesheni,kuweka jiwe la msingi,i ujenzi wa kituo cha afya Mzinga ,kukagua na kuweka la uzinduzi kituo cha afya Kivule,kukagua na kuweka mradi wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Ukonga.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema asilimia 80 ya mapato Tanzania yanatokana na Wilaya ya Ilala ambayo unaongoza kukusanya mapato katika nchi hii aliwataka wananchi wa wilaya ya Ilala wampigie kura Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mwezi Octoba .

Kwa upande wake Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala Mhandisi John Chacha Magori,akizungumzia mradi wa ujenzi wa barabara ya Magengeni, Changombe shule ya Afrikan ,Sanene yenye urefu wa KM 0.5 moja ya barabara zinazotekelezwa na Serikali ambao unahusisha barabara za Faru,Mnyamani, KM O .39,Sukita 0.5 Km , Mwanza 0.37.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa Isimail Ally Ussi ,alisema barabara ya Tabata Magengeni imeleta mageuzi makubwa Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, nawapongeza barabara hii imezingatia sifa zote na imekizi vigezo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge Isimail Ally Ussi aliwataka wananchi wa Segerea kuitunza barabara hiyo ambapo aliwataka wananchi wa Segerea wasitupe takataka katika mifereji .

Kwa upande mwingine Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Isimail Ally amemwagiza Mkandarasi wa barabara hiyo kuweka taa za barabarani na kuzingatia kwani barabara hiyo imezingatia sifa za matumizi ya fedha za Serikali .

Mwenge wa Uhuru ulianza mbio zake Mkoa Dar es Salaam Juni Mosi ukitokea Mkoani Lindi ambapo Juni Mosi ulizindua miradi ya maendeleo Wilayani Temeke na Juni pili ulizindua miradi ya maendeleo wilaya ya Kigamboni Juni tatu imezindua miradi ya maendeleo Wilayani Ilala.