Wakenya hususan wale wanaoishi Mjini Nairobi hii leo siku ya Ijumaa watapata fursa ya kuuaga mwili wa Raila Odinga kwa siku ya pili mfululizo katika uwanja wa Nyanyo Jijini Nairobi.
Hatua hii inajiri baada ya Serikali Kutangaza siku kuu ya Raila siku ya ijumaa ili kutoa fursa ya kuuaga mwili wa marehemu.
Kulingana na ratiba ya mazishi iliotolewa na serikali, kutakuwa na na ibada ya mazishi mapema leo kabla ya mwili wake kuagwa.
Naibu rais Kithure Kindiki anayeongoza ratiba ya mazishi ya kiongozi huyo maarufu nchini Kenya amesema kwamba Wageni ikiwemo viongozi wa mataifa jirani Afrika na wale wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Amewasihi Wakenya kuwasili katika uwanja huo mapema zaidi kuanzia saa tatu asubuhi ili kuzuia ghasia kama zile zilizoshuhudiwa katika uwanja wa kasarani.
Siku ya Alhamisi watu watatu wlifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika machafuko yaliyozuka katika uwanja wa Kimataifa,
Kasarani, ambapo maelfu ya Wakenya walikuwa wamekusanyika kutoa heshima zao za mwisho
