Muungano wa kijeshi wa NATO unaratibu ufikishaji wa kawaida wa silaha kubwa kwa Ukraine baada ya Uholanzi kusema itatowa mfumo wa ulinzi wa anga, risasi na msaada mwengine wa kijeshi wenye thamani ya euro milioni 500.

Sweden pia ilitangaza siku ya Jumanne (Agosti 5) kwamba itachangia dola milioni 275 kwenye juhudi za pamoja na majirani zake wa Denmark na Norway ili kukamilisha kitita cha dola milioni 500 kwa mifumo ya ulinzi wa naga, silaha za kushambulia vifaru, risasi na vipuri.

Awamu mbili za ufikishaji wa vifaa, sehemu kubwa ikiwa inatoka Marekani, zinatazamiwa kuwasili Ukraine mwezi huu, ingawa msaada kutoka mataifa ya Nordic unatazamiwa kuwasili mwezi Septemba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na NATO, utumwaji wa silaha hizo ni kwa mujibu wa matakwa ya Ukraine inayopambana na uvamizi wa Urusi kwa mwaka wa tatu sasa.