Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Jumapili Agosti 31 ,2025 ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mkutano mkubwa katika mji wa Nyamongo, jimbo la Tarime vijijini mkoani Mara.

Balozi Dkt.Nchimbi pia aliwanadi wagombea Wabunge wa majimbo ya Mkoa huo akiwemo mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijini,Mwita Waitara pamoja na madiwani

Dkt.Nchimbi ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.