Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia wananchi wa kata ya Katoro , leo Jumamosi Septemba 6,2025 Wilaya ya Geita, Mkoani Geita .
Dkt Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani Geita leo, kusaka kura za ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),akitokea mkoani Shinyanga.
Maara baada ya kuwahutubia wananchi wa jimbo la Katoro, Dkt Nchimbi aliwanadi wagombea Ubunge,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Katoro,Mhandisi Kija Limbu Ntemi pamoja na Madiwani.









