Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es Salaam
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo , na maofisa ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kwa kusoma katiba ,Sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo.
Agizo hilo limetolewa Dar es Salaam Julai 21, 2025 na Mjumbe wa Tume huru ya Uchaguzi Balozi Omar Ramadhan Mapuri wakati wa ufungnzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wapatao 108 kutoka Halmashauri za Bagamoyo, Mkuranga, Rufiji, Chalinze za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

” Mafunzo haya yakakwenda ni kwa lengo la kusoma katiba , sheria na maelezo mbalimbali yanayotolewa na Tume Ili mnapotoka hapa muweze kuogoza na kusimamia vyema uchaguzi utakao kuwa huru na haki” amesema.
Hata hivyo Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imetenga siku hizi tatu kuwapatia mafunzo haya kama sehemu ya kuwaongezea maarifa na uzoefu kwenye kipindi chote cha uchaguzi mkuu kwa kuzingatia Sheria na kanuni za uchaguzi .
Sanjari na hayo sheria na miongozo kwa wasimamizi wa uchaguzi inawataka wapiga kura kutoka kwenye maeneo ya kata na mikoa kushiriki zoezi la upigaji kura linapaswa kuwa la haki kwa raia wa Tanzania.

Aidha ameipongeza INEC na jukumu la kusimamia pamoja na kuratibu uendeshaji wa chaguzi kwa mujibu wa Sheria kulinda Democrasia kwa manufaa ya wananchi , vyama vya siasa vyote na wagombea
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume hiyo, Giveness Aswile, amesema mafunzo hayo yalipangwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza yalifanyika Julai 15 hadi 17, na awamu ya pili ya kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.

