WAZIRI Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kwamba kampeni yake dhidi ya Iran “itabadili sura ya Mashariki ya Kati”, wakati nchi hizo mbili zikiendelea kushambuliana vikali kwa siku ya tano.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza kwamba kampeni yake dhidi ya Iran “itabadili sura ya Mashariki ya Kati”, wakati nchi hizo mbili zikiendelea kushambuliana vikali kwa siku ya tano.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu jioni, Netanyahu alisema kuwa Israel inawaondoa viongozi wa kiusalama wa Iran “mmoja baada ya mwingine” na kwamba kwa kufanya hivyo wanabadili “sura ya Mashariki ya Kati, na hilo litaleta mabadiliko makubwa ndani ya Iran yenyewe”.

“Tumeua safu ya juu ya viongozi wa usalama wa Iran, wakiwemo wakuu watatu wa kijeshi. Kamanda wao wa jeshi la anga, wakuu wawili wa kijasusi. Jana, tulimuua mwingine wa jeshi na jeshi la walinzi wa Mapinduzi. Tulimlenga mkuu wa kitengo chao cha operesheni. Tunamwondoa mmoja baada ya mwingine,” alisema Netanyahu.

Wakati Netanyahu akitoa kauli hizo, Iran nayo imeendelea kuvurumusha makombora dhidi ya Israel, huku Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran likijigamba kwamba mashambulizi yataendelea “bila kukatizwa hadi alfajiri.”