Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kutokana na changamoto ya ajira inayowakumba vijana nchini, Kampuni ya Norland, inayojihusisha na utafiti, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa tiba za afya, imejipanga kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wote wa Kitanzania, ili kuwasaidia kujipatia kipato halali kwa matumizi yao binafsi na familia zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Norland, Mr. Benno Mwitumba, alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kuanzisha mpango wa kuwawezesha vijana kupata ajira ili kupunguza wimbi la wategemezi na kuongeza tija katika jamii kwa kuwa mawakala wa bidhaa hiyo yenze uhitaji sana hapa nchini .

“Kuna idadi kubwa ya vijana mitaani wasiokuwa na ajira za kudumu. Sisi tuko tayari kuwapatia fursa ambapo watafanya kazi na kujilipa kulingana na bidii zao binafsi,” alisema Mr. Mwitumba.

Aidha, Mr. Mwitumba alisema kuwa kampuni yao inaleta bidhaa za kiafya ambazo zinalenga kutibu chanzo cha tatizo katika mwili wa binadamu, na kwamba bidhaa hizo zimeonesha mafanikio makubwa kwa watumiaji ndani na nje ya nchi.

“Dawa, vyakula na vinywaji vinavyoingia mwilini kwa sasa vimetengeneza sumu na usugu unaosababisha miili kuwa dhaifu au tegemezi. Bidhaa zetu husaidia kurejesha afya bila kutegemea dawa nyingine za muda mrefu,” aliongeza.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na waandishi wa habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George Simbachawene, alibainisha kuwa Serikali haiwezi kutoa ajira kwa kila mhitimu wa chuo kikuu kila mwaka, na hivyo alihimiza sekta binafsi kushiriki katika kutoa ajira kwa vijana.


Waziri Simbachawene aliwataka vijana kuchangamkia fursa za kujiajiri, hasa kupitia sekta ya kilimo na ujasiriamali, badala ya kutegemea ajira za Serikali ambazo ni chache kwa idadi.

“Kutokana na changamoto hizo zilizobainishwa na Mheshimiwa Waziri, sisi kama Norland tunatoa fursa kwa vijana wote nchini kujiunga nasi ili wauze bidhaa zetu za afya. Watapata kipato kikubwa kulingana na juhudi zao na mzunguko wa biashara wanayoifanya,” alifafanua Dkt. Mwitumba.

Kwa upande wake, Mwekezaji Mkuu wa Norland nchini, Bw. Samuel Ikongwe, alisema huu ni wakati sahihi kwa vijana kujijenga kiuchumi kwa ajili ya maisha yao ya sasa na ya baadaye.

“Tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini. Serikali inafanya kazi nzuri kwa nafasi yake, nasi kama sekta binafsi tunachukua jukumu la kusaidia wale waliokosa ajira za Serikali kwa kuwapatia fursa ya kujipatia kipato kupitia biashara ya bidhaa zetu,” alisema Bw. Ikongwe.

Norland ni kampuni yenye makao makuu nchini China, na makao makuu ya kimataifa nchini Marekani. Kampuni hiyo huzalisha zaidi ya bidhaa 40 za afya, na kwa sasa ipo katika zaidi ya nchi 50 duniani kote.

Nimeongoza Uzinduzi wa Maonyesho ya Ajira ya Nne (4) ya Tanzania na China yaliyofanyika katika Viwanja vya Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam , Dar Es Salaam. Maonyesho hayo ambayo yanalenga kutangaza na kuwaunganisha Vijana wahitimu na wenyeujuzi Watanzania na makampuni ya Kichina yanayofanya kazi Nchini Tanzania.

Maonyesho hayo ambayo yanalenga kuwaunganisha vijana wa Kitanzania na fursa za Ajira nimeyafungua kwa kuwakumbusha umuhimu kuenzi ushirikiano uliopo wa nchi zetu mbili na hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto ya ajira nchini. Maonyesho haya yanataraji kutoa fursa za Ajira zaidi ya ajira 2000.

Mhe. Kikwete amesema maonesho hayo ni kati ya hatua za serikali ya Awamu ya Sita katika kutatua changamoto ya Ajira nchini, ambapo kupitia maonesho hayo makampuni ya China yanayofanya kazi hapa nchini yanaonesha mahitaji yao ya ujuzi wanaohitaji ili vijana wakitanzania weweze kuchangamkia fursa hizo.

Hivyo vijana wenye sifa za mahitaji ya makampuni hayo kufuatia makubaliano baina ya serikali zetu katika kufikia maendeleo endelevu ambayo nchi yetu itafaidika katika shughuli za makampuni hayo nchini na kuwapa nafasi vijana wazawa wenye sifa wanazohitaji.

Katika hatua nyengine nimewahakikishia watanzania kuwa serikali kupitia ofisi hiyo itaendelea kuratibu kwa tija masuala ya ajira nchini huku tukisimamia maslahi mapana ya Watanzania kqma ilivyoelekezwa nq sheria, sera na miongozo ya Ajira na Kazi na maono yq Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.