Na Mwandishi wetu, Jamhuti, Media, Dar es Salaam

Katika hali inayoonesha bidhaa zake kukubalika na watanzania wengi kampuni ya Norland Tanzania ambayo makao makuu yake yapo nchini Chna,imejipanga kujitanua na kuhakikisha inaendelea kutoa elimu kuhusiana matumizi ya bidhaa zao za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho yanayoendelea ya Saba Saba jijini Dar es Salaam, Mkurugenz Mkuu wa Norland,Bw Benno Mwitumba amesema kuwa mpaka sasa shuhuda nyingi zinaonesha watu wengi wamenufaika na bidhaa za afya za Norland.

“Umma huu uliokusanyika hapa hapa ni ishara tosha kuwa bidhaa hizi ni kielelezo cha ubora wake na mafanikio katika kutatua changamoto mbalimbali za kiafya”, alisema Bw Mwitumba.

Bw Mwitumba alisema bidhaa za Norland zimeweza kutatua matatizo ya kiafya ya wagonjwa mbalimbali waliokuwa na matatizo ya kansa, tezi dume, kuziba kwa mirija ya uzazi kwa akina mama, kwa kutatua changamoto hizo wameweza kuendelea na shughuli zao za kila siku za kiuchumi, wakati hapo awali walikwamishwa kutokana na changamoto hizo.

Aidha, Bw Mwitumba alisema kuwa wanapokea simu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ambao wanapata taarifa za bidhaa zao za afya, na kuwafanya waweze kufungua ofisi katika mikoa mbalimbali nchini.

“Tutaanza kufungua ofisi zetu katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kwa kuanza na mkoa wa Mbeya pamoja na mikoa jirani ili kuwa karibu na wagonjwa na kujipatia huduma hii kwa ukaribu zaidi”, alisema Bw Mwitumba.

Mwekezaji Mkuu wa Kampuni ya Norland inayojihusisha na utafiti ,uzalishaji na usambazaji wa bidha za afya za tiba asili, Bw. Samuel Ikongwe (kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Norland Bw. Benno Mwitumba kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha utumiaji wa bidhaa za norland kwa wanachama wapya, wakati wa wa kilele cha sikukuu ya Sabasaba, yaliyokuwa na kaulimbiu isemayo ijue norland badilisha maisha.

“Nipende kutoa wito kwa watanzania wote wenye changamoto mbalimbali za kiafya na wamejaribu kutumia tiba mbalimbali lakini bado hawajapata matokeo mazuri, waje Norland na watarudisha tabasamu lao kama wagonjwa wengine wengi ambao wamepata matibabu kwetu na kubadilisha maisha yao”, alisema.

Bw Mwitumba aliwashauri wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi Mkuu ujao wa Oktoba 2025 kutumia bidhaa za afya za Norland kwani zitawapa nguvu na kuwaondolea uchovu wa ziara pamoja na kuondoa sumu mbalimbali katika miili yao.

Kwa upande wake, Muwekezaji Mkuu wa Kampuni hiyo nchini, Bw Samuel Ikongwe alisema kuwa kupitia maonesho hayo ya Saba Saba, wamepata picha halisi ya wahitaji wa bidhaa za afya kutoka kwa wagonjwa wa mikoa mbalimbali na kutangaza kuwa wataanza kupeleka huduma hiyo katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Tumepokea mrejesho kutoka katika mikoa mbalimbali wakihitaji huduma yetu kwa kiasi kikubwa, hivyo basi uongozi umeona tuna kila sababu yakuanza kufungua ofisi zetu katika mikoa ya Mbeya, Iringa. Njombe na Songwe.

Hata hivyo, Bw Ikongwe aliwataka Watanzania wazingatie kanuni bora za afya ili kuepuka kupata maradhi ya kuduma, kwani gharama zake ni kubwa kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzinunua.

Naye Dkt Stanley Mapunda, ambaye ni Mwananchama wa kampuni hiyo alisema kuwa amekuwa shuhuda wa wanaume wengi ambao walikuwa na wanasumbuliwa na maradhi ya tezi dume na kusabisha kupata maumivu na kushindwa kufurahia faragha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Norland Bw. Benno Mwitumba akitoa elimu kwa vitendo kwa wanachama wapya juu ya matumizi ya bidhaa za afya za tiba asili za kampuni hiyo wakati wa kilele cha sikukuu ya sabasaba yaliyokuwa na kaulimbiu isemayo ijue norland badilisha maisha

“Wanaume wengi hawana utamaduni wa kupima afya zao, mimi leo nawashauri wajijengee tabia ya kupima afya zao ikiwemo tezi dume katika hatua za mwanzo haina dalili, watakaokutwa na changamoto hii, waje watumie bidhaa za Norland zitaondoa changamoto hiyo”, alisema Dkt Mapunda.

Naye Genoveva Miluko aliyejiunga na kampuni hiyo miaka mitatu iliyopita alisema kuwa ameweza kuwatibu watu wengi ambao walikuwa na changamoto mbalimba;li za kiafya hasa kwa upande wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ya kudumu.

“Mara baada ya kuhitimu chuo kikuu nilikaa muda mrefu bila ajira, nikaamua kujiunga na Norland na ninathubutu kusema kuwa nimepata mafanikio makubwa hasa katika kuwatibu wagonjwa mbalimbali” alisema

Bi Miluko alielezea mafanikio mengine aliyoyapata ni pamoja na kuajiri vijana katika ofisi yake, na hiyo ni kutokana na kazi nzuri ya Norland, hata hivyo aliwasihi vijana wajitokeze kwa wingi katika kujishuhulisha na biashara mbalimbali ikiwemo ya Norland yenye faida kubwa.