Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Katika harakati za kuboresha afya ya Watanzania kwa kutumia njia mbadala zisizo na madhara, kampuni ya Norland imeendelea kuleta mapinduzi kupitia virutubisho vyake vya asili vinavyolenga kusafisha miili na kuimarisha kinga ya mwili kwa asilimia mia moja.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Norland, Bw Benno Mwitumba, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kutumia bidhaa za tiba lishe zinazotengenezwa kwa viambato vya asili, akisisitiza kuwa bidhaa hizo haziangalii tu dalili za magonjwa, bali hutatua chanzo chake kabisa.

“Katika aiosha yetu ya kawaida, tumekuwa tukila vyakula na kutumia dawa nyingi za kisasa kwa muda mrefu, na nyingi kati ya hizo zimeacha sumu mwilini,”
“Hali hii imesababisha miili kuwa dhaifu na hivyo kuwa rahisi kushambuliwa na maradhi kila mara. Lazima tuusafishe mwili wetu ili kurudisha uimara wa kiafya na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nchi yetu tukiwa na afya njema,” alisema Bw Mwitumba.
Kwa mujibu wake, Norland imejikita katika kutengeneza virutubisho lishe ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa wengi katika mataifa mengi duniani ikiwemo China na Marekani katika kupambana na maradhi yasiyoambukiza yanayoendelea kusababisha athari kubwa katika jamii.
“Changamoto nyingi za kiafya huanzia tumboni. Hapa ndipo sumu hujikusanya na kusababisha matatizo mengine mwilini. Sisi hatutibu tu dalili, bali tunashughulikia chanzo chake,” aliongeza.
Virutubisho hivyo, ambavyo tayari vimeanza kupata umaarufu nchini baada ya kufanyiwa utafiti wa kutosha na kuthititishwa na Mamlaka ya Viwango nchini (TBS), vimeelezwa kuongeza kinga ya mwili maradufu, kuimarisha mfumo wa usagaji chakula, na kusaidia mwili kujitibu wenyewe bila kutegemea dawa kali za kemikali.
Bw Mwitumba pia alipongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na saratani, akisema Norland iko bega kwa bega kusaidia katika mapambano hayo.
“Tunaishukuru sana Serikali katika kuisadia Norland kupata ithibati hapa nchini ili kuwa suluhisho la matatizo ya kiafya kwa Watanzania ili washiriki vizuri katika ujenzi wa taifa,”
“Hata wakati tunaomba ithibati hakutupata urasimu wowote katika kupata vibali vya kuendesha shughuli zake hapa nchini baada ya TBS kukagua ubora wa bidhaa za asili Norland na kujiridhisha kuwa salama kwa Watanzania na tiba kwa magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza,” amesema na kuongeza; .
“Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Hii ni hatua kubwa,”
“ Zamani ilihitaji subira sana, lakini sasa imekuwa tofauti na ndio maana tumeamua kuwekeza hapa nchini katika tiba lishe kwa Watanzania ,”alisema Bw Mwitumba.

Kwa sasa, Norland inazidi kupanua wigo wake nchini Tanzania kwa kuwafikia Watanzania wengi zaidi vijijini na mijini, huku ikitangaza uwepo wa fursa kwa vijana kuwa mawakala wa bidhaa zake katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
“Kutokana na uhitaji wa bidhaa zetu, tumeamua kutangaza fursa kwa watu wa rika zote hasa vijana kujiingizia kipato kwa kuwa mabalozi wetu,” amesema.
kwa upande wake wakala Mkuu na Mwekezaji wa Norland hapa nchini, Bw Samuel Ikongwe amesema shuhuda zimekuwa nyingi watu wengi waliotumia bidhaa hizo na kufurahia matokeo yake.
Amesema Norland yenye makao yake makuu nchini China imeleta mafanikio makubwa katika sekta ya afya na kuwa mkombozi mkubwa kwa watu waliokwisha kata tamaa,” alisema Bw Ikongwe.
Amewataka watazania kutumia virutubusho vya Norland ambayo imetafiti na kutengeneza zaidi ya aina tofauti arobaini,” alisisitiza.
