Julius Nyerere: Kufikiri unajua kila kitu ni hatari

“Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja ya kujifunza tena. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.”

 

Maneno haya ni ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Ndiye Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania.

 

 

Malkia Elizabeth I: Sipendi anayejali umalkia wangu pekee

 

“Sipendi mwanaume anayeniheshimu kama malkia, kama hanipendi kama mwanamke.”

 

Haya ni maneno ya Malkia Elizabeth I wa Uingereza na Ireland, anayefahamika pia kama Malkia Bikira.

 


Ngugi wa Thiong’o: Viongozi Afrika wanawanyima watu fursa

 

“Kansa iliyopo katika vichwa vya viongozi wetu barani Afrika kuwa maendeleo ya nchi zao hayawezi kufikiwa bila kujua lugha ya Kiingereza ni mbaya kwa kuwa inawanyima watu fursa nzuri ya kuelewa mambo mengi yanayoendelea duniani.”

 

Hii ni kauli ya mtunzi gwiji wa vitabu barani Afrika, Profesa Ngugi wa Thiong’o, ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Marekani.

 

 

Janet Yellen: Kukosa ajira muda murefu ni hatari

 

“Kutoajiriwa kwa kipindi kirefu kunaweza kumfanya mfanyakazi yeyote kuwa chini ya maendeleo ya kuajiriwa, hata baada ya uchumi kuimarishwa.”

 

Maneno haya ni ya Janet Yellen, mchumi na profesa wa nchini Marekani, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa shirikisho linalofahamika kama FRS nchini humo.

By Jamhuri