JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Dk. Lwaitama: Tuboreshe, tusivunje Muungano

Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari  uliojiweka wazi  katika taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na mwandishi wa gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la Agosti 7, 2012), Datus Boniface.  Huyu mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa  walithubutu kusema uongo kuwa  eti “ Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof Shivji waliushambulia Muungano.” Tena, mwandishi huyu na wahariri walioruhusu habari hiyo ichapishwe  wakaenda mbali zaidi na kutumia  kichwa  cha habari kilichosema eti ‘Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe’.

Yah: Mwongozo wa Spika, lini serikali itahamia Dodoma?

Wanangu, leo ni siku nyingine ya Jumanne katika wiki hii ambayo ni nadra sana kuifikia, kama hujui kwamba kesho ni mtihani mkubwa kwako kutokana na siri kubwa aliyonayo Mwenyezi Mungu juu yako; ni yule ambaye si muumini wa dini yoyote ndiye anayeweza akawa kichaa asijue hilo. Nimefarijika mno na demokrasia inayoendelea hapa nchini kwa mambo ambayo kama si kigezo, yanaweza yakatutoa siku moja hapa tulipo na kutupeleka kule tutakako kwa nia njema na ya dhati kutoka kwa hao waitwao watawala wenye nia njema ya maendeleo.

Madai ya Tundu Lissu yachunguzwe

Katika gazeti la leo kuanzia ukurasa wa kwanza tumechapisha ripoti maalum yenye kuonyesha hali ya wasiwasi katika muhimili wa tatu wa dola uliokasimiwa jukumu la msingi la kutoa haki. Wasiwasi huu umeibuliwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge.

RIPOTI MAALUMU

Majaji ‘vihiyo’ watajwa

*Yumo aliyeshindwa kuandika hukumu miaka minne

*Wengine wagonjwa, hawajawahi kusikiliza kesi

*Yumo Jaji wa Mahakama ya Rufaa asiye na shahada

*Baada ya kubanwa sasa anasoma Chuo Kikuu Huria

*Wengine walikuwa mahakimu watuhumiwa wa rushwa

 

Kagasheki akimweza huyu, ataweza kila kitu

 

Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), aliubua bungeni mkataba ulioingiwa baina ya kampuni za Uranium Resources PLC, Western Metals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited, mkataba ambao umetengenezwa na kampuni ya Kitanzania ya Rex Attorneys na kusainiwa Machi 23, 2007.

Wabunge waunga mkono msimamo wa Morocco

Bunge la Tanzania linaunga mkono msimamo wa Morocco katika kupata ufumbuzi wa mgogoro kati ya taifa hilo na taifa la Sahara Magharibi. Mwaka 1975 uliibuka mgogoro wa ndani kati ya Morocco na taifa la Sahara Magharibi linalotaka kujitangazia Uhuru. Mgogoro huu uliofanya Sahara Magharibi kujenga ukuta kama wa Berlin kule Ujerumani, umekuwa na madhara makubwa ndani ya taifa la Morocco.