JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

MAANDIKO YA MWALIMU NYERERE

‘Kutegemea kubaya kupita kote ni kutegemea mtu mwingine kwa mawazo

Katika sehemu iliyopita, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema hata angekuwa anafuata sera za kibepari, angejenga viwanda. Anasema mabepari ndiyo walioanza kujenga viwanda, na viwanda vyenyewe havikuwa na sera. Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu aliyoitoa katika kilele cha Sherehe za Mei Mosi, mwaka 1995 mkoani Mbeya.Juzi

Rais Kagame si wa kumwamini sana

Makala iliyopita ya “JWTZ nginjangija Goma hadi Kigali’, imenifumbua macho. Nimepata simu nyingi na ujumbe wa maandishi usio idadi. Wapo waliotumia lugha kali, lakini wengi walikuwa waungwana. Hiyo ndiyo raha ya mijadala. Kuna wakati tunaweza kukubaliana kwenye baadhi ya mambo, na wakati mwingine tusikubaliane kwa hoja fulani fulani. Muhimu ni kujenga moyo wa uvumilivu na staha.

Sote tukiwa waoga nchi itayumba

Ni kosa kubwa kwa mtoto wa Kizanaki kumtamkia mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Hawa ni tofauti na makabila mengine, mathalani Wajita. Wao mtoto ana uhuru na haki ya kumtamkia mzazi au mtu aliyemzidi umri neno ‘mwongo’. Wakati Mzanaki atapambana kumnasa vibao mtoto anayeamini kamtukana, mzazi wa Kijita atafanya juhudi za kupambana kwa hoja kumthibitishia mtoto yule kwamba yeye (mkubwa) si mwongo. Hizo ni tofauti za wazi kwa makabila hayo mawili.

Messi alipa faini ya kukwepa kodi

Nyota wa timu ya soka ya Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi pamoja na baba yake mzazi wamelipa euro milioni tano, sawa na dola milioni 6.6 za Marekani, baada ya kubainika na kosa la kukwepa kodi. Messi na mzazi wake huyo walidaiwa kukwepa kulipa kodi hiyo ya serikali kwa njia za ujanjaujanja.

Kambi ya upinzani walitoka na hoja zao

Wiki iliyopita, Mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulikuwa na vibweka na vimbwanga vingi vyenye kuacha kinywa wazi kwa mshangao na hamaki kwa mtu yeyote makini mwenye kuujali mustakabali mwema wa nchi yake.

Hata hivyo, pamoja na vibweka na vimbwanga vilivyotokea kwenye kikao hicho, ukweli unabaki kuwa kilikuwa kikao chenye moja ya miswada muhimu yenye kipekee unaokwenda kuweka jiwe jipya la msingi kwa Tanzania tunayoihitaji kuijenga kwa miaka 50, au hata 100 ijayo.

KAULI ZA WASOMAJI

 

Tunaandaa vichaa, maskini