Latest Posts
Chakula cha bure: Falsafa ya Pinda!
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaisimamia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ili igawe chakula cha bure kwa kaya 20,000 zinazoishi katika Tarafa ya Ngorongoro.
Muhongo akagua ujenzi bomba la gesi
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kuridhishwa kwake na kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Mil 121/- ‘zatafunwa’ Hospitali ya Geita
Siri ya wizi wa Sh zaidi ya milioni 121 za Hospitali ya Wilaya ya Geita imefichuliwa. Imewekwa wazi na aliyekuwa Mhasibu wa Idara ya Afya hospitalini hapo, Frank Maganga, akimtaja aliyekuwa Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Omary Dihenga, kutumia…
Vidonda vya tumbo na hatari zake (16)
Wiki iliyopita, Dk. Khamis Zephania alieleza vyanzo na madhara ya magonjwa ya saratani ya tumbo na vidonda vya tumbo kwa mama wajawazito. Sasa mfuatilie zaidi katika sehemu hii ya 16…
Jinsi vidonda vya tumbo vinavyochunguzwa
Salaam za Kagasheki kwa majangili
*Angependa wakikutwa maporini ‘wamalizwe’ huko huko
*Maelfu ya wananchi wakubali adhabu ya kifo kwa wahusika
*Muswada kuipa makali sheria kuwasilishwa Bunge lijalo
Muda ni saa 2 na dakika kadhaa asubuhi. Mbele ya Makao Makuu ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuna mamia ya watu wa rika, rangi na jinsi zote. Wana mabango yenye ujumbe maalumu.
Dola ikomeshe vibaka kwenye daladala
Tatizo la vibaka limeendelea kuota mizizi katika daladala za abiria, hasa jijini Dar es Salaam. Baadhi ya watu wanaotumia usafiri huo wa umma wamekuwa wakiibiwa fedha na simu za kiganjani kila kukicha!