Papa Leo XIV ameongoza Misa katika Kanisa la Sistine, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo kama kiongozi wa Kanisa Katoliki.
Alibusu madhabahu na kuizunguka mara moja akiwa na moshi wa ubani.
Papa aomba msamaha wa Mungu
Ibada hiyo imeanza kwa maombi yaliyoongozwa na Papa, ya kukiri dhambi na kuomba msamaha wa Mungu.
Papa Leo amehutubia Makardinali, akianza hotuba yake kwa Kiingereza.
Anasema wamemwita ili abarikiwe na utume wa kuliongoza Kanisa.
“Najua ninaweza kumtegemea kila mmoja wenu kutembea nami tunaposonga mbele kama Kanisa, jumuiya ya marafiki wa Yesu, kama waumini, kutangaza habari njema, kutangaza Injili,” alisema.
