Papa Leo alionya dhidi ya “matumizi ya nguvu kiholela” na “uhamisho wa kulazimishwa wa watu” wa Gaza katika mazungumzo ya simu na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas siku ya Jumatatu, kulingana na taarifa kutoka Vatican.
Papa pia alisisitiza haja ya haraka ya “kutoa msaada kwa wale walio hatarini zaidi kutokana na mzozo na kuruhusu kuingia kwa misaada ya kutosha ya kibinadamu”, ilisema taarifa hiyo.
Wiki iliyopita, Papa Leo alisisitiza tena wito wake wa kusitisha mapigano Gaza baada ya watu watatu waliokuwa wakihijifadhi katika kanisa katoliki katika mji wa Gaza kuuawa kwa shambulizi la Israel.
Telegramu ilisema Papa “amehuzunishwa sana kujua kuhusu kupoteza maisha na majeraha yaliyosababishwa na shambulio la kijeshi” kwenye Kanisa la Holy Family.
