Risala za pongezi bado zinaendelea kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kanisa Katoliki kumchagua kiongozi wake mkuu – Leo XIV.

Papa Leo wa 14 amechaguliwa wakati ambapo nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imekosa usalama kwa miongo kadhaa sasa.

Idadi kubwa ya watu nchini humo ambao wengi wao ni Waumini wa Kanisa Katoliki wanahisi Papa mpya atachangia pakubwa katika upatikanaji wa amani katika eneo la mashariki mwa Congo.

”Mimi nasema Mungu amtie nguvu na aisaidie kwa maombi nchi yetu ina vurugu sana, nchi yetu haina amani inayokumbwa na vita’’, alisema mmoja wa waumini.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo linaongoza kwa kuwa na waumini wengi barani Afrika.

Baadhi yao walikuwa na matumaini Papa mpya atatokea Congo.