WAZIRI Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Taifa, Mizengo Pinda amewataka waliopewa dhamana ya kusimamia mchakato wa uteuzi wa wagombea kwenye chama hicho kutenda haki.

Pinda amesema kwa kufanya hivyo wataweza kuondoa malalamiko kwa watia nia lakini na wanachana na kupata wagombea ambao wataweza kuwa na sifa zinazostahiki.

Pinda alitoa kauli hiyo jana alipotembelea ukarabati wa jengo la chama hicho Mko wa Tanga.

Alisema kuwa kazi iliyokuwepo ya upande wa chama ni kuhakikisha tunapata wagombea ambao wataweza kupokelea vizuri kwa wananchi.

“Lazima tupate wagombea ambao ni wazuri watakaoweza kupambana na makundi mengine ya vyama vingine vya siasa hivyo mchuje mgombea ambao atweza kuketa ushindani wakati wa uchaguzi mkuu utakapofika,” alisema Pinda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman alisema kuwa ukarabati wa ofisi hiyo ni sehemu ya maelekezo ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Rais Samia.

“Rais samia alitoa maelekezo ya kuhakiki mali za chama lakini majengo yaliyopo yaweze kukarabatiwa ili yaweze kuendana na hadhi ya chama hicho,” alisema.