Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kupatikana kwa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo hapa nchini kumewasaidia wananchi wengi kupata huduma hizo kwa wakati na hivyo kuokoa maisha yao.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo linalofanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

Pinda alisema kabla ya kupatikana kwa huduma hizo hapa nchini wagonjwa wengi walikuwa wanatibiwa nje ya nchi kwa gharama kubwa lakini hivi sasa huduma zinapatikana ndani ya nchi na kupunguza gharama ya kuzifuata nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akisoma folder lenye taarifa za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za upimaji wa moyo zinazotolewa katika zoezi la kupima magonjwa hayo   linalofanyika katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

“Nimewahi kupata huduma ya kupima na kutibiwa afya ya moyo JKCI na Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) huduma nilizopata ni nzuri na za kiwango cha kimataifa kwani wana mashine za kisasa za kupima na kutibu moyo pia kuna wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu”.

“Ninaipongeza JKCI na BMH kwa huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa ambazo zimesaidia kuokoa maisha ya wagonjwa, pia ninawapongeza watoa huduma za matibabu ya moyo kwa kuokoa maisha ya watu”, alisema Mhe. Pinda.

Mhe. Pinda aliwahimiza wananchi kujenga tabia ya kupima afya za mioyo yao mara kwa mara hasa pale zinapotokea kambi maalumu za matibabu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo ambazo hazina gharama zaidi ya mtu kutenga muda wa kwenda kupima.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge aliishukuru serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika tiba ya moyo hapa nchini na kusababisha Tanzania kuwa kivutio cha utalii tiba barani Afrika.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Galiyaya akimpima kiwango cha sukari kwenye damu Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Ole Shangai aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

Dkt. Kisenge alisema taasisi hiyo itaendelea kutoa huduma za upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi kwa kuwafuata mahali walipo ili wananchi wengi wafikiwe na huduma za kibingwa za matibabu ya moyo.

“Huduma hii tunayoitoa hapa Bungeni inajulikana kwa jina la Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services ambapo tangu imeanza mwishoni mwa mwaka juzi tumeona zaidi ya watu 22,000 katika mikoa 22”, alisema Dkt. Kisenge.

Kwa upande wa wananchi waliopata huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo walishukuru kwa huduma waliyoipata na kusema kuwa imewasaidia kufahamu afya za mioyo yao.

“Nimefika katika banda la JKCI nimepata huduma ya upimaji wa viashiria vya magonjwa ya moyo, ushauri wa jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo pamoja na lishe bora ninashukuru huduma niliyoipata ni nzuri”, alisema Mhe. Emmanuel Ole Shangai Mbunge wa Ngorongoro.

Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimpima uwiano baina ya urefu na uzito Mbunge wa Momba Mhe. Condester Sichalwe aliyetembelea banda la taasisi hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo zinazotolewa katika viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

“Huduma niliyoipata ni nzuri nimepima vipimo vya urefu, uzito, wingi wa sukari kwenye damu, shinikizo la damu na kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi na nimepewa ushauri wa lishe na jinsi ya kujiepusha na magonjwa ya moyo”, alisema Chiku Ramadhani Mfanyakazi wa Bunge.

“Ninawashauri wafanyakazi wenzangu waje kupima na kujua afya za mioyo yao kwani magonjwa ya moyo yanatibika kama yatagundulika mapema lakini ukichelewa gharama za matibau zinakuwa kubwa na wakati mwingine unaweza usipone kabisa” alisema Chik