Na Mwandishi Wetu, Jamhuri Media, Uvinza
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambaye ni mratibu wa kampeni wa chama hicho mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi, amewataka wananchi wa Kigoma kutokubali watu wanaotishia amani ya nchi kuwalaghai.
Pinda ametoa kauli hiyo Leo Septemba 13,2025 katika viwanja vya Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma alipopewa nafasi ya kusalimia maelfu ya wananchi mbele ya mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan.
Amewataka wananchi wa mkoa huokujitokeza Kwa wengi kwenda kupiga kura ili waongoze kwa kutoa kura nyingi za ndiyo kuliko mikoa mwingine.
‘ Tunataka ushindi wa kishindo, Lazima tuwe wamoja na wenyewe mshikamano mkubwa
“Kigoma mna matawi 8,826, nakiomba chama kupitia matawi na wilaya twendeni chini kwa wapiga kura kule chini, huko tutajihakikishia ushindi, twendeni chini,”amesema.
Pia aliwashukuru wabunge kwa kufanya kazi nzuri na kuendelea kuwa wamoja baada ya kuteuliwa, hivyo kuwatakila waendelee kuwa mshikamano huo.
Amesema chama kinapoamua kimeamua kinaamha kwa moyo safi . ” Yaliyopita si ndwere tugang yajayo”amesema.
