Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kupitia Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu imetupilia mbali pingamizi dhidi ya mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo, Bi. Rosemary Kasimbi Kirigini.
Pingamizi hilo liliwasilishwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi CCM, Salum Khamis Salum, kwa barua ya tarehe 27 Agosti 2025. Hata hivyo, baada ya kupitia utetezi wa Bi. Rosemary, Msimamizi wa Uchaguzi Eng. Elieza Reuben Mayengo alitoa uamuzi kwamba mgombea huyo ana sifa za kuendelea kugombea ubunge, kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024 pamoja na ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa uamuzi huu, Bi. Rosemary Kasimbi Kirigini ataendelea na safari yake ya kuwania ubunge katika Jimbo la Meatu kupitia tiketi ya ACT-Wazando.
