Katika Mkoa wa Dodoma, juzi Desemba 8, 2025 wananchi walifurika katika eneo la Soko Kuu la Majengo kununua mahitaji mbalimbali kufuatia hofu ya maandamano yaliyokuwa yametangazwa kufanyika Desemba 9. Hadi saa mbili usiku, soko hilo lilikuwa limejaa watu wengi waliokuwa wakinunua bidhaa mbalimbali zikiwemo nyanya, viazi mviringo, ndizi za kupika , karoti, hoho, sukari na mboga za majani kwa wingi.
Siku iliyofuata, Desemba 9, hali ya amani iliendelea kudumu, ambapo vikosi vya JWTZ pamoja na polisi walionekana wakipita katika mitaa na maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
Hata hivyo, maduka mengi pamoja na wajasiriamali wadogo walifunga biashara zao tofauti na ilivyo katika siku nyingine za maadhimisho ya Uhuru ambapo hata kama hakuna sherehe za kitaifa, wananchi huendelea na shughuli zao za kiuchumi kama kawaida.
Aidha kwa mujibu wa taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi ,Hadi muda wa machana siku ya Disemba 9,2025 mchana ,Hali ya Usalama wa Nchi ilikuwa shwari.
Aidha ilisema vyombo vya ulinzi na Usalama vinaendelea kuimarisha Usalama nchini sambamba na kulinda maisha ya watu na Mali zao .


