Jeshi la Polisi lingependa kueleza kuwa, kuna hii picha mjongeo ya zamani na nyinginezo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikihadaa wananchi kuwa maandamano yameshaanza.

Hakuna jambo kama hilo kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo mitaani kudhibiti hali kama hiyo kama kuna ambao watakaidi kuelewa katazo lililotolewa Desemba 5,2025 kwa mujibu wa sheria za nchi.

Jeshi la Polisi Tanzania linaendelee kusisitiza kuwa, kinacho hamasishwa na kuitwa maandamano ya amani yasiyo na kikomo bado yamepigwa marufuku kwa sababu hayajafuata na wala hayajakidhi matakwa ya Sheria Mama ambayo ni Katiba ya Mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura 322.

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma,Tanzania