Jeshi la Polisi limeona picha mjongeo inayosambaa katika mitandao ya kijamii akionekana mwanamke mmoja akimhamasisha na kumnywesha pombe mtoto mdogo jambo ambalo ni ukatili kwa mtoto na ni kinyume na sheria za nchi.

Sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Mtoto Sura ya 13 na Urekebu wa mwaka 2023 kifungu cha 9 (3) na 13 pia ukisoma Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 na Urekebu wa mwaka 2023 kifungu cha 169 A.

Ufuatiliaji wa kina umeshaanza kama tukio hili limetokea ndani ya nchi yetu ili kuweza kumpata huyu aliyekuwa anafanya kitendo hicho kama inavyoonekana kwenye picha mjongeo hiyo.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa yeyote anayemfahamu huyu mwanamke asisite kutupatia taarifa kwa njia yeyote ile ambayo anaona inafaa na ni rahisi kwake au kupitia namba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi 0699 998899.

Aidha tunamtaka mwanamke huyu akiona taarifa hii ajisalimishe mwenyewe katika kituo chochote cha Polisi.