Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linawashikilia waandishi wa habari wawili Julius Msagati wa EATV na Given Mashati wa A24 waliokuwa mkoani humo kufuatilia upigaji kura za maoni ngazi ya udiwani leo eneo la Mererani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Ahmed Makarani amesema wanawashikiliwa waandishi hao kwa mahojiano na baada ya kuhojiwa wataachiwa.

Tukio hilo limezua maswali miongoni mwa wadau wa habari kuhusu uhuru wa vyombo vya habari wakati wa michakato ya kisiasa. 📸 Katika picha: Kulia ni Julius Msagati wa EATV, na kushoto ni Given Mashati wa A24.