Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema yuko tayari kukutana na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky mjini Moscow. Pia ameapa kuendelea kupigana na Ukraine kama makubaliano ya amani hayatofikiwa.

Pia Putin ameapa kuendelea kupigana na Ukraine kama makubaliano ya amani hayatofikiwa.

Aliyasema hayo juzi mwishoni mwa ziara yake nchini China wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyakisema ana matumaini ya kuzungumza na Rais wa Marekani Donald Trump ili kushinikiza kuiwekea Urusi vikwazo vipya.

Ameyaelezea matumaini hayo mjini Copenhagen anakohudhuria mkutano wa kujadili msaada wa ziada kwa ajili ya Ukraine kutoka nchi za Baltiki na Skandinavia.

Mkutano huo unajiri wakati viongozi wa Ulaya wakitarajiwa kukutana kesho Alhamisi mjini Paris kujadili hakikisho la usalama kwa Ukraine.