Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema siku ya Jumatatu kuwa vikosi vya Urusi vinapata ushindi katika kile alichokiita “vita vya haki” nchini Ukraine.
Putin alisema hayo kwenye video iliyochapishwa katika tovuti ya Ikulu ya Kremlin na kuongeza kuwa wapiganaji na makamanda wa Urusi wanaendeleza mashambulizi na nchi nzima ya Urusi inapigana vita hivyo vya haki na kufanya kazi kwa bidii.
Alisema kwa pamoja wanatetea upendo walionao kwa ardhi ya Urusi pamoja na mshikamano kuelekea hatima yao ya kihistoria na kusisitiza kuwa wanapigana na wanashinda.
Urusi hadi sasa inadhibiti karibu kilomita za mraba 114,500 sawa na asilimia 19 ya Ukraine ikiwa ni pamoja na Rasi ya Crimea na majimbo mengine makubwa yaliyoko mashariki mwa Ukraine.
