Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Kibaha
Mkoa wa Pwani unaendelea kuonyesha mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na sekta mbalimbali, amesema Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mkoa huo, Pili Mnyema, ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa.
Mnyema aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi Mkoa wa Pwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kibaha.
Alihimiza ushirikiano, nidhamu, uadilifu, uwajibikaji na kufanya kazi kwa bidii katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Niwaombe tuendelee kushirikiana ili kuendeleza mafanikio ,”Niwapongeze kwa mafanikio yaliyofikiwa, kwani Mkoa wa Pwani unaongoza katika mambo mengi yaliyoiwezesha kuwa kinara katika sekta mbalimbali”
Aidha, alitaka mkoa kuipa kipaumbele ajenda ya uwekezaji, huku akibainisha kuwa Mkoa wa Pwani ni mkoa wa kimkakati katika uwekezaji wa viwanda.
Kikao hicho kilipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026 na kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya mwaka 2026/2027.






