Raia wawili wa China wanatuhumiwa kuingiza nchini Marekani kuvu ambayo maafisa wanasema ni “kiini hatari cha kibaolojia”.

Yunqing Jian, 33, na Zunyong Liu, 34, wameshtakiwa kwa kula njama, kusafirisha bidhaa, kutoa taarifa za uongo na ulaghai wa viza, Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani wa Michigan ilitangaza Jumanne.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa Bw Liu alijaribu kuingiza kuvu hiyo n chini kupitia uwanja wa ndege wa Detroit ili aweze kuofanyia utafiti katika maabara ya Chuo Kikuu cha Michigan ambako mpenzi wake, Bi Jian, alifanya kazi.

Kuvu inayofahamika kisayansi kama Fusarium graminearum inasababisha magonjwa kwa mimea ya ngano, shayiri, mahindi na mchele ambayo inaweza kuangamiza mazao na kusababisha kutapika na uharibifu wa ini ikiingia kwenye chakula.

Kuvu hiyo kisayansi ni kama “silaha inayoweza kuwa ya ugaidi wa kilimo”, kulingana na Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani, ikiongeza kuwa inaweza kusababisha hasara ya “mabilioni ya dola kote duniani kila mwaka.”

Maafisa zaidi wanadai kuwa Bi Jian alipokea ufadhili kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya utafiti wake kuhusu ugonjwa huo nchini China. Pia wanadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China.

Mwanasheria wa Marekani Jerome F Gorgon Jr alielezea madai hayo kama “wasiwasi mkubwa zaidi wa usalama wa taifa”.

“Wageni hawa wawili wameshtakiwa kwa kusafirisha kuvu ambayo imefafanuliwa kama ‘silaha inayoweza kutumika kama ugaidi wa kilimo’ katika eneo la Marekani, inaonekana walikusudia kutumia maabara ya Chuo Kikuu cha Michigan kuendeleza mpango wao.”

Uchunguzi huo ulikuwa juhudi za pamoja kati ya FBI naIdara ya Forodha ya Marekani na Ulinzi wa Mipaka.

BBC imewasiliana na Chuo Kikuu cha Michigan na ubalozi wa China mjini Washington DC kwa maoni.