Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Mzee Cleopa David Msuya yatakayofanyika Kesho Kijijini kwake Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro, tarehe 13 Mei, 2025.