Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo la Kigongo, Misungwi mkoani Mwanza tarehe 19 Juni, 2025. Daraja hilo ambalo ni sehemu ya barabara ya Usagara-Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Sirari hadi Mtukula na ujenzi wake ulianza rasmi mwezi Februari, 2020.